Terms za kutumia
Version 2026-10-v1
1. Sisi ni akina nani
ZAMU Defence inaendeshwa na HK Law, firm ya mawakili Kenya.
2. Maelezo ya bure ni info ya sheria
Maelezo ya bure hupangwa automatically na AI kutoka kwa charge sheet na majibu yako, ikitumia sheria za criminal za Kenya zinasimamiwa na HK Law. Ni info ya sheria ya jumla. Si legal advice ya case yako specifically, na kuitumia hakufanyi HK Law kuwa wakili wako.
3. Packs za kulipia ni kazi yenye mipaka
Ukinunua pack unaagiza HK Law kwa hiyo pack pekee. Wakili anachekia, anarekebisha na kuapprove kila kitu kabla ukipate. Hii haijumuishi kufika kotini ama kukutetea zaidi ya pack, isipokuwa utuagize separately. Fee ya kila pack inaonyeshwa kabla ulipe na unapewa fee note.
4. Hakuna guarantee
Maamuzi ya bail, kama ako guilty na sentence hufanywa na korti. Hakuna mtu anaweza guarantee matokeo.
5. Responsibility zako
Toa info ya ukweli na ucheki charges tumesoma ukilinganisha na karatasi. Usitumie hii service kujaribu kuinfluence witness ama complainant, kuficha ama kutengeneza evidence, ama kuhepa korti — hatutasaidia na hizo.
6. Tukishindwa kukusaidia
Kabla wakili achekie pack ya kulipia, tunahakikisha HK Law haina conflict of interest. Tukishindwa kukusaidia, tutakuambia na tukurudishie doh yote. Huenda tusiweze kukuambia sababu.
7. Mambo ya haraka
Kama mtu ako cells ama ako na kotini ndani ya siku mbili, tupigie — usingoje app. 0708111222