ZAMU DefenceHK Law

Privacy notice

Version 2026-10-v1

HK Law ndio data controller wa ZAMU Defence chini ya Data Protection Act, 2019.

Kile tunachukua

Namba yako ya simu na jina; picha za charge sheet (ziko na majina ya watu wengine, kama complainant); charges; majibu yako kwa maswali yetu; na details za malipo kutoka M-Pesa.

Mbona

Ni ya kukueleza case yako tu, kupanga packs unanunua, kucheki conflict of interest, kupokea malipo na kukucheki kuhusu case yako. Hatuuzi data yako wala kuitumia kwa ads.

AI inayofanya kazi nje ya Kenya

Picha na majibu yako hutumwa kwa AI provider wetu, ambaye servers zake ziko nje ya Kenya, ili kusoma charge sheet na kupanga maelezo. Tunazituma tu ukikubali, wakati unaingia.

Tunaiweka kwa muda gani

Case za bure hujidelete siku 90 baada ya kuzitumia mara ya mwisho. Ukinunua pack ama uagize HK Law, case inakuwa part ya file ya client kwa firm na inawekwa vile sheria inataka kwa files za mawakili.

Rights zako

Unaweza omba kuona, kurekebisha ama kudelete data yako, na unaweza delete case ya bure mwenyewe kutoka kwa page ya case. Tuandikie service@hklaw.co.ke. Pia unaweza complain kwa Office of the Data Protection Commissioner.

Security

Picha zinawekwa nje ya website ya public na zinaonyeshwa kwako tu na kwa staff wa HK Law wanashughulikia case yako. SMS zetu hazitaji charge kamwe.